Kuhusu Toto Smart

Toto Smart ilianza nyumbani-kutoka kwa mzazi aliyetamani kuona mtoto wake akijifunza kwa furaha, vitendo, na ubunifu.

Baada ya kuona changamoto ya vifaa vya kujifunzia vinavyofaa, visivyoegemea skrini, na vinavyoheshimu maadili ya kiafrika, tulianza kutengeneza vifaa rahisi vya kujifunzia kwa mikono. Kupitia vipande vya maboksi yaliyotumika, mbao, shanga/visoda, na vitu mbalimbali tunavyotumia mazingira ya nyumbani, kupitia ubunifu, watoto hujifunza kufikiri, kutatua matatizo, na kujitegemea.

Toto Smart huunda vifaa/nyenzo za kujifunzia vinavyofanya elimu iwe ya kufurahisha, tulivu, na yenye maana-bila presha, bila skrini, na kwa kuzingatia ukuaji wa akili, mikono, na tabia njema.

Toto Smart-Mahali mikono midogo hujenga akili kubwa.